Home Sports KMC YAPOTEZA KWA MARA NYINGINE TENA

KMC YAPOTEZA KWA MARA NYINGINE TENA

IKIWA ugenini leo Februari 25 imepoteza kwa mara nyingine tena ukiwa ni mchezo wa ligi.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Azam FC 1-0 KMC.

Ni mchezo wa pili mfululizo KMC kupoteza ikiwa Dar katika msako wa pointi tatu ikiwa inaongozwa na nahodha Emmauel Mvuyekule.

Ilitoka kunyoshwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ikiwa nyumbani Februari 22 na leo Februari 25 imepoteza mbele ya Azam FC.

Bao la ushindi limefungwa na Idd Suleiman, ‘Nado’ dakika ya 52 kwenye mchezo huo.

Katika mchezo mwingine ni Coastal Union imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Previous articleHUYU HAPA MFUNGAJI WA BAO LA SIMBA KIMATAIFA
Next articleSIMBA YASEPA NA POINTI TATU KIMATAIFA