Home Uncategorized HUYU HAPA MFUNGAJI WA BAO LA SIMBA KIMATAIFA

HUYU HAPA MFUNGAJI WA BAO LA SIMBA KIMATAIFA

BAO la kwanza kwenye anga za kimataifa kwa Simba hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa limefungwa Uganda.

Ni Henock Inonga anafunga bao hilo dakika ya 19 akiwa ndani ya 18 kwenye harakati za kutimiza majukumu yake.

Ni pasi ya Moses Phiri ameitumia beki huyo kuipa uongozi Simba dhidi ya Vipers.

Moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa huku tatizo la umakini likiendelea kuikumba Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiungo Clatous Chama na Saido Ntibanzokiza bado hawajaonesha ubora wao ndani ya dakika 45 za mwanzo.

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA VIPERS YA UGANDA
Next articleKMC YAPOTEZA KWA MARA NYINGINE TENA