Home Uncategorized AZAM FC KUSHUKA UWANJANI NA MABINGWA

AZAM FC KUSHUKA UWANJANI NA MABINGWA

FEBRUARI 14 2023 kikosi cha Azam FC kilifanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuwakabili mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2023 leo Februari 15,2023.

Mlandege ambao waliwashangaza mabingwa watetezi Simba pamoja na watani zao wa jadi Yanga kushuhudia wakitwaa ubingwa leo wanakibarua cha kumenyana na Azam FC.

Ni mchezo wa kirafiki ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Utakuwa ni mchezo wa pili kwa Azam FC kucheza ule wa awali ilikuwa dhidi ya KMKM na walipata ushindi wa ao 1-0 Uwanja wa Azam Complex.

Kali Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema wanatumia muda kufanya maandalizi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zao zijazo.

“Tunafanya maandalizi kwa ajili ya mechi zetu na tunaamini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Mchezo wao ujao kwenye ligi ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 21.

Previous articleZIGO ZITO WAPEWA MANULA, BOCCO, CHAMA
Next articleFEISAL NYOTA WA YANGA APATA AJALI