Home Sports ZIGO ZITO WAPEWA MANULA, BOCCO, CHAMA

ZIGO ZITO WAPEWA MANULA, BOCCO, CHAMA

MASTAA wa Simba ikiwa ni pamoja na John Bocco, Clatous Chama,Aishi Manula, Pape Sakho, Shomary Kapombe wamepewa zigo zito kuhakikisha wanapambana kupata matokeo kwenye mechi zote za hatua ya makundi.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira akishirikiana na Juma Mgunda ilianza kwa kuambulia kichapo ugenini ubao uliposoma Horoya 1-0 Simba mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bao hilo walifungwa ndani ya dakika 20 za kipindi cha mwanzo na Pape Ndiaye aliyemtungua Manula dakika ya 18 na lilidumu mpaka mwamuzi alipokamilisha mchezo huo.

Kituo kinachofuata kwa Simba kwenye hatua ya makundi kundi C ni mchezo dhidi ya Raja Casablanca unaotarajiwa kuchezwa Februari 18, Uwanja wa Mkapa.

Mgunda amesema kuwa wamepata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wote kuwaambia kuwa kinachotajika ni matokeo mazuri kwenye mechi ambazo wanacheza.

“Kwenye mechi za hatua ya makundi tumewaambia wachezaji kuwa malengo ya awali tulipokuwa tukicheza kwenye zile hatua za mwanzo ilikuwa kufika hatua ya makundi ambayo tupo hivyo ni lazima tuondoke eneo hili tusonge mbele.

“Timu imecheza hatua ya robo fainali hivi karibuni na sasa ina malengo yake ambayo ni kufanikiwa kufika mbali tofauti na wakati uliopita, vijana wameelewa na kwa msaada wa Mungu tunaamini kila kitu kitakuwa sawa,”.

Baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Horoya ugenini timu ya Simba jana ilifanya mazoezi ya mwisho na kufanya maandalizi ya kurejea Tanzania ambapo wanatarajiwa kuwasili leo.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Raja Casablanca unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 18.

ReplyForward

Previous articleYANGA WAMECHOREWA RAMANI YA KUTUSUA CAF
Next articleAZAM FC KUSHUKA UWANJANI NA MABINGWA