Home Uncategorized ISHU YA FEI TOTO IWE DARASA KWA WACHEZAJI WENGINE

ISHU YA FEI TOTO IWE DARASA KWA WACHEZAJI WENGINE

KWENYE ulimwengu wa michezo moja ya mjadala ambao unafuatiliwa pia licha ya kuwa na mambo mengi ni pamoja na sakata la Feisal Salum.

Wimbo huu umeimbwa kwa muda huku kila pande ikivutia kwake huku kila mmoja akihitaji haki yake.

Ukiweka kando masuala ya mvutano bado ukweli upo wazi kwamba kwa namna ambavyo hali ipo kwa yule ambaye anahitaji kufanya maamuzi yake kuna utaratibu ambao upo.

Suala la kuvunja mkataba ama kupewa mkataba lina kanuni zake hizi ni lazima zifuatwe kwa kila mmoja iwe ni muajiri pamoja na yule muajiriwa.

Inapofika muda wa kutaka kuvunja mkataba husika pia taratibu zipo kwa namna ilivyo inaonyesha kwamba kuna mahali hapakuwa sawa jambo linaloleta mvutano kwa sasa.

Mchezaji kuingia kwenye mvutano na timu yake ni hasara kwake na timu kuingia kwenye mvutano na mchezaji ni hasara pia.

Kinachotakiwa kwa wachezaji wengine kulichukua suala hili kuwa somo kwao kwani inapofika wakati wa usajili imekuwa na mvurugano.

Mvurugano wa haya mambo unapoteza muda kwa wachezaji kushindwa kuwa kwenye ubora hasa pale wanaposhindwa kufanya mazoezi pamoja na timu.

Pia itakuwa ni ngumu kwa mchezaji kurejea kwenye ubora wake akiwa nje ya uwanja kwa muda bila kuwa kwenye program na wachezaji wengine.

Hakuna anayependa kuona mvutano unatokea lakini maslahi ni jambo la msingi kuzingatiwa kwa pande zote huku utaratibu ukifuatwa na kila pande.

Previous articleMGUNDA KWA REKODI HII ANASTAHILI PONGEZI
Next articleSINGIDA BIG STARS NI WAMOTO KWELIKWELI