Home Sports SINGIDA BIG STARS YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

SINGIDA BIG STARS YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

SINGIDA Big Stars wana jambo lao ndani ya Kombe la Mapinduzi kutokana na kasi yao mbele za vigogo wanaokutana nao.

Inakuwa timu ya kwanza kwenye makundi msimu huu kushusha kichapo kikubwa na mchezaji wake mmja kufunga mabao yote baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC.

Ni Francis Kazad ambaye ni ingizo jipya ndani ya Singida Big Stars ametupia mabao yote manne.

Ilikuwa ni dakika ya 27,53,64 na 86 huku bao pekee la Azam FC likifungwa na Abdul Suleiman, ‘Sopu’.

Sasa Singida Big Stars inatinga hatua ya fainali Kombe la Mapinduzi 2023 inamsubiri mshindi wa nusu fainali kati ya Namungo v Mlandege.

Namungo wao ilipenya hatua ya nusu fainali mbele ya Aigle Noir huku Mlandenge wao wakipenya kwenye kundi baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Simba kundi C.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan ambapo Mlandege ni timu pekee kutoka Zanzibar iliyopenya kwenye hatua ya nusu fainali kati ya sita kutoka visiwani hapo.

Michuano hii ya historia imekuwa ikifanyika tangu 2007 na fainali inatarajiwa kuchezwa Januari 13,2023.

Previous articleMUDATHIR AAHIDI MAPAMBANO YANGA
Next articleKULIA MAYELE,KUSHOTO KUNA HIKI CHUMA