Home Sports MUDATHIR AAHIDI MAPAMBANO YANGA

MUDATHIR AAHIDI MAPAMBANO YANGA

KIUNGO mpya wa Yanga, Mudathir Yahya, ameweka wazi kuwa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, kina wachezaji wazuri jambo linalomfanya azidi kupambana.

Ingizo hilo jipya ndani ya Yanga, mchezo wake wa kwanza kucheza ilikuwa dhidi ya KMKM katika Kombe la Mapinduzi 2023 ambapo aliingia dakika ya 77 kuchukua nafasi ya Clement Mzize.

Kwenye mchezo huo, Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Dickson Ambundo. Mchezo wa pili Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars ambapo Mudathir alianza kikosi cha kwanza.

Mudathir amesema: “Yanga ina wachezaji wazuri na mimi pia nipo ndani ya kikosi chenye wachezaji wazuri, ninaamini kwamba tutapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu.”

Previous articleALIYEKUWA KWENYE HESABU ZA SIMBA HUYO KWA WAKULIMA
Next articleSINGIDA BIG STARS YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI