Home Sports ALIYEKUWA KWENYE HESABU ZA SIMBA HUYO KWA WAKULIMA

ALIYEKUWA KWENYE HESABU ZA SIMBA HUYO KWA WAKULIMA

DILI la kijana Kelvin Nashon kutua ndani ya mitaa ya Kariakoo limegonga mwamba na sasa atakuwa kwa wakulima wa alizeti.

Nashon ambaye ni kiungo alikuwa kwenye hesabu za Yanga na Simba lakini ameibuka ndani ya Singida Big Stars.

Simba walikuwa wanahitaji kuongeza kiungo mkabaji atakayeongeza nguvu katika kikosi hicho ila wamemkosa nyota huyo.

Leo Januari 8,2023 nyota huyo yupo kwenye kikosi cha nusu fainali Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC ambapo anajiunga na timu hiyo akitokea Geita Gold.

Previous articleKOCHA MPYA SIMBA AANZA KAZI NAMNA HII
Next articleMUDATHIR AAHIDI MAPAMBANO YANGA