Home Uncategorized MITAMBO YA PENALTI SIMBA HII HAPA

MITAMBO YA PENALTI SIMBA HII HAPA

 SIMBA imekamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2022/23 huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 31.

Kweye mabao hayo ni mawili yamefungwa kutokana na penalti ilikuwa dhidi ya Geita Gold ambapo mtupiaji alikuwa ni Clatous Chama.

Aliyesababisha penalti hiyo ni Augustino Okra kisha penalti ya pili ilikuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga walipocheza na Coastal Union.

Mbele ya Coastal Union timu ambayo imetengenezwa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ambaye anainoa Simba kwa sasa ilisababishwa na Shomari Kapombe.

Kapombe ndani ya ligi katupia bao moja kibindoni akiwa ni mzee wa kumwaga maji na ana pasi moja ya bao.

Kwa mapigo ya faulo ndani ya kikosi cha Simba ni Clatous Chama na ni kinara wa pasi za mwisho akiwa nazo 8 ndani ya ligi.

Katupia mabao mawili kibindoni msimu huu wa 2022/23 kwenye ligi.

Previous articleHAZARD ASTAAFU MAJUKUMU YA TIMU YA TAIFA
Next articleMAYELE, MGUNDA WASEPA NA TUZO NOVEMBA