Home International HAZARD ASTAAFU MAJUKUMU YA TIMU YA TAIFA

HAZARD ASTAAFU MAJUKUMU YA TIMU YA TAIFA

EDEN Hazard nyota wa timu ya Real Madrid ameamua kustaafu kutumika majukumu ya Timu ya Taifa ya Ubelgiji baada ya timu hiyo kufungashiwa virago kwenye Kombe la Dunia hatua ya makundi huko Qatar,2022.

 Nahodha huyo wa timu ya taifa amefunga jumla ya mabao 33 kwenye mechi 126 ambazo amecheza na timu hiyo tangu akiwa na miaka 14.

Hazard alikamilisha majukumu yake kumaliza wakiwa ni washindi wa tatu kwenye Kombe la Dunia 2018 lakini mwaka huu mambo yamekuwa magumu.

Nyota huyo ameandika kupitia Ukurasa wake wa Instagram kuwa:”Asante kwa upendo wenu, asanteni kwa sapoti yenu ambayo mmekuwa nayo na asante kwa yote ambayo yametokea tangu 2008.

“Nimeamua kufikia mwisho kwenye masuala ya Timu ya Taifa, maamuzi tayari nimeyafikia na nitawakumbuka kwelikweli.

Timu hiyo ilikuwa kundi F na mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco ulileta mvurugano kwao baada ya ubao wa Uwanja wa Al Thumama kusoma Ubelgiji 0-2 Morocco ambapo watupiaji kwa Morocco walikuwa ni Romain Saiss dakika ya 73 na Zakaria Aboubkal dakika ya 90.

Timu ya Morocco kutoka Afrika imetinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Hispania na kuandika rekodi ya kutinga kwenye hatua hiyo kwa mara ya kwanza.

Hispania ilishinda kwa mikwaju ya penalti 3-0 ambapo wanatarajiwa kumenyana na Timu ya Taifa ya Ureno ambayo nayo ilitinga hatua hiyo mara ya mwisho kutinga hatua ya robo fainali ilikuwa ni 2006.

Previous articleMSHAMBULIAJI HUYU KUMALIZANA NA SIMBA
Next articleMITAMBO YA PENALTI SIMBA HII HAPA