Home Sports MAYELE, MGUNDA WASEPA NA TUZO NOVEMBA

MAYELE, MGUNDA WASEPA NA TUZO NOVEMBA

NYOTA wa Yanga Fiston Mayele amechaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya TFF imeeleza kuwa haikumuhusisha kocha wa Azam FC kwa kuwa timu hiyo haikuwa na kocha mkuu kwa Novemba.

Ikumbukwe kwamba Azam FC ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 8 na kashinda zote.

Mayele katupia kambani mabao 10 na ametoa pasi moja ya bao, ndani ya Novemba Mayele alitupia mabao saba kwenye mechi za ligi.

Aliwashinda Moses Phiri wa Simba pamoja na Said Ntibanzokiza wa Geita Gold ambao aliingia nao fainali.

Kwa upande wa Kocha Bora wa mwezi tuzo imesepa na Juma Mgunda ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba.

Mgunda aliwashinda Hans Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Maxime wa Kagera.

Meneja bora wa wa Uwanja wa Liti uliopo Singida, Hussein Simba amechaguliwa kuwa meneja bora kwa Novemba.

Previous articleMITAMBO YA PENALTI SIMBA HII HAPA
Next articleMTAMBO WA MABAO WAREJEA AZAM FC