Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO WAREJEA AZAM FC

MTAMBO WA MABAO WAREJEA AZAM FC

 NDANI ya kikosi cha Azam FC namba moja kwa utupiaji ni Idris Mbombo ambaye ametupia mabao sita kibindoni.

Hakuwa kwenye mechi za mwisho za mzunguko wa ligi kwa kuwa hakuwa fiti lakini tayari kwa sasa ameanza mazoezi kwa ajili ya kurejea uwanjani mzunguko wa pili.

Miongoni mwa mechi ambayo alikosekana ni ile yakufungia mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja waUshirika, Moshi uliposoma Polisi Tanzania 0-1 Azam FC na mtupiaji alikuwa ni Ayoub Lyanga.

Azam FC chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala imekuwa kwenye mwendo bora ambapo mechi zote nane ambazo alikaa benchi ilisepa na ushindi.

Msako wa pointi 24 kwenye ligi nyumbani na ugenini alikomba pointi zote na timu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 35.

Mchezo ujao wa Azam FC ni kwenye Kombe la Shirikisho ambapo watacheza na Malimao FC raundi ya Pili, Uwanja wa Azam Complex, Desemba 9.

Previous articleMAYELE, MGUNDA WASEPA NA TUZO NOVEMBA
Next articleSIKU SITA TU, BONGE LA BEKI LINAKUJA, AZAM WANAMTAKA FEI TOTO