
IHEFU WAIVUNJA REKODI YA YANGA KWENYE LIGI
WAKULIMA kutoka Mbeya, Ihefu FC wamevunja mwiko wa Yanga kuendelea kucheza mechi za ligi bila kufungwa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1. Wakiwa Uwanja wa Highland Estate, Ihefu walianza kutunguliwa bao kipindi cha kwanza kupitia kwa kiraka Yanick Bangala dakika ya 8. Ni Nivere Tigere aliweka usawa dakika ya 38 na kuwafanya waende mapumziko…