Home Sports NYOTA HAWA YANGA KUIKOSA IHEFU

NYOTA HAWA YANGA KUIKOSA IHEFU

KIUNGO wa Yanga, Bernard Morrison anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Ihefu utakaochezwa Uwanja wa Highland Estate.

Nyota huyo ataungana na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na Feisal Salum, Heritier Makambo ambao hawajawa fiti.

Nyota hawa walikosekana pia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku mtupiaji akiwa ni Fiston Mayele.

Pia Feisal alikosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano ambayo imegota mwisho lakini kwa sasa bado hajawa fiti.

Fei alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Liti na alikwama kuyeyusha dakika 90.

Cedric Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo wa leo na wanaamini watapambana kupata matokeo licha ya kuwakosa wachezaji wengine.

“Wapo wachezaji ambao tutawakosa lakini haina maana kwamba tutashindwa kuwa kwenye ule ubora ambao tunataka hasa pointi tatu,”

Previous articlePHIRI KAVUNJA REKODI MBOVU SIMBA
Next articleKOCHA JUMA MGUNDA ATAJA UGUMU ULIPO