Home Sports PHIRI KAVUNJA REKODI MBOVU SIMBA

PHIRI KAVUNJA REKODI MBOVU SIMBA

MOSES Phiri nyota wa Simba amevunja rekodi yake ya kushindwa kufunga nje ya Dar kwenye mechi za ligi ambazo alicheza msimu huu wa 2022/23.

Kibindoni Phiri ana mabao 8 ambapo sita alifunga Uwanja wa Mkapa aliwafunga bao mojamoja Geita Gold,Kagera Sugar,KMC,Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar na Namungo.

Nje ya Dar ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, ubao uliposoma Prisons 0-1 Simba kwa bao la Jonas Mkude na mchezo dhidi ya Mbeya City sare ya kufungana bao 1-1 hizi zilichezwa Uwanja wa Mkapa na ubao wa Liti uliposoma Singida Big Stars 1-1 Simba, mechi hizi zote Phiri hakufunga.

Aliibuka kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Ushirika alipofunga mabao mawili na kufikisha mabao 8 wakati timu hiyo iliposhinda mabao 3-1.

Simba inafikisha pointi 31 kibindoni baada ya kucheza mechi 13 kwenye msimamo wa ligi ni namba tatu huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 32 baada ya kucheza mechi 12.

Mchezo ujao ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga unoatarajiwa kuchezwa Desemba 3,2022, Mkwakwani, Tanga.

Previous articleYANGA:MECHI DHIDI YA IHEFU NI NGUMU
Next articleNYOTA HAWA YANGA KUIKOSA IHEFU