Home Uncategorized YANGA:MECHI DHIDI YA IHEFU NI NGUMU

YANGA:MECHI DHIDI YA IHEFU NI NGUMU

CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa mechi yao dhidi ya Ihefu ni ngumu kuliko mchezo wa Dabi.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Highland Estate.

Yanga imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City na mabao yote yalifungwa na Fiston Mayele mwenye mabao 10 kibindoni.

“Kucheza na timu ambayo ipo kwenye nafasi kama iliyo Ihefu ni ngumu zaidi ninaweza kusema kuliko kucheza Dabi kwa kuwa Dabi mchezaji hahitaji kupewa maelekezo zaidi bali ni kuongezewa kidogo.

“Hapa ninaona tupo kwenye mtego na ambacho tunapaswa kukifanya ni kutegua mtego huo hicho ndicho ambacho tumewaambia wachezaji wetu,” amesema.

Kwenye msimamoa Ihefu ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 8 baada ya kucheza mechi 13 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 32 baada ya kucheza mechi 12.

Previous articleBRAZIL YAPENYA JIONI KABISA KOMBE LA DUNIA
Next articlePHIRI KAVUNJA REKODI MBOVU SIMBA