Home International BRAZIL YAPENYA JIONI KABISA KOMBE LA DUNIA

BRAZIL YAPENYA JIONI KABISA KOMBE LA DUNIA

 USHINDI wa bao 1-0 Uswisi ambao wamepata timu ya taifa ya Brazil mbele ya Uswisi umewapa tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2022, Qatar.

Bila ya staa wao Neymar Brazili imetinga hatua ya 16 bora kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mwanzo mwisho Uwanja wa 974.

Dakika ya 83 bao hilo limefungwa na kuwafanya Brazil kuongoza kundi G wakiwa na pointi sita kibindoni.

Mchezo huo wa kundi G ulishuhudiwa na mashabiki 43,649 ambapo Casemiro alipachika bao hilo lililomuibua Neymar aliyeumia enka kwenye mchezo wa ufunguzi katika kundi hilo wakati wakishinda dhidi ya Serbia.

Washindi hao mara tano wa Kombe la Dunia walipata tabu kuvunja ngome ya wapinzani wao ambao waliweka ukuta mgumu, zikiwa zimebaki dakika 7 kugota 90wakafanikiwa kupata bao la ushindi kupitia kwa kiungo Casemiro.

Ikumbukwe kuwa bao la mapema dakika ya 64 lililofungwa na staa wao Vinicius Jr ambaye alikuwa chini ya uangalizi mkubwa na mabeki wa Uswisi lilifuntwa baada ya VAR kutazamwa na kuonekana kwamba ilikuwa ni mtego wa kuotea.

Brazili inaongoza kundi G ikiwa na pointi 6 itamenyana na itamenyana na Cameroon ya Afrika kwenye mchezo wa mwisho ampoa  ili Cameroon itinge hatua ya 16 bora ni lazima ishinde mchezo huo.

Ikiwa nafasi ya tatu na pointi moja ina kazi ya kusubiri matokeo ya wapinzani wao Uswisi wenye pointi tatu nafasi ya pili kwakuwa wakishinda mchezo wao dhidi ya Serbia wanasonga mbele hatua ya 16 bora.

Hivyo ili Cameroon isonge mbele chaguo lao ni kushinda dhidi ya Brazil na kuona Serbia ikishinda mbele ya Uswisi.

Kazi kubwa kwa Ghana kutoka Afrika kupata ushindi mbele ya timu hiyo kwenye mchezo wa mwisho huku Uswisi nao wakiwa wanahitaji ushindi mchezo wao wa mwisho dhidi ya Serbia.

Previous articleURENO YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA
Next articleYANGA:MECHI DHIDI YA IHEFU NI NGUMU