Home International URENO YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

URENO YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

TIMU ya taifa ya Ureno imetinga hatua ya 16 bora kwenye Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uruguay.

Mbele ya mashabiki 88,668 mashabiki walishuhudia mabao yote yakifungwa na Bruno Fernandes ambaye alikuwa kwenye ubora wake.

Dakika ya 54 na 90 alipachika bao hilo kwa mkwaju wa penalti na kuifanya timu hiyo kuongoza kwenye kundi H.

Kwenye mchezo huo Uruguay walikosa nafasi ya kufunga ikiwa ni pamoja na ile aliyokosa Maxi Gomez baada ya shuti lake kugonga mwamba na baadaye Luis Suarez naye alikosa nafasi ya kufunga.

Cristiano Ronaldo alikosa nafasi ya kufunga baada ya kupishana na krosi iliyopigwa na Bruno dakika ya 54 na ikajaa mazima nyavuni ikiwa ni bao la uongozi kwa Ureno.

Fernandes alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90+3 baada ya VAR kuamua kuwa ni penalti kwa kuwa mchezaji wa Uruguay Gimenez alionekana kuushika mpira huo.

Ureno inatinga hatua ya 16 bora ikiungana na Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi pamoja na Brazil ambao nao wamekata tiketi ya kutinga 16 bora kwenye Kombe la Dunia 2022, Qatar.

Bado ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya Korea Kusini huku Ghana ya Afrika iliyo nafasi ya pili ikiwa na mchezo dhidi ya Uruguay, Ijumaa Novemba 30.

Mechi hizo za Novemba 30 ni za maamuzi kwa timu ya pili itakayouungana na Ureno hatua ya makundi kutoka kwenye kundi H kwa kuwa Ghana ina pointi tatu ikiwa nafasi ya pili na Korea Kusini na Uruguay hizi zina pointi mojamoja, zikipoteza mechi zao za mwisho basi watarejea nyumbani.

Ghana ikishinda dhidi ya Uruguay ina uhakika wa kusonga mbele lakini kwa Korea Kusini ikipoteza haitakuwa na chaguo sawa na Uruguay pia.

Previous articleISHU YA KOCHA MPYA MSIMBAZI IMEFIKIA HAPA
Next articleBRAZIL YAPENYA JIONI KABISA KOMBE LA DUNIA