Yanga Yakaribia Kumnasa Oumar Farouk Comara Kutoka Golden Arrows

Yanga SC inaendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, huku ikiwa hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki wa kati wa klabu ya Golden Arrows, raia wa Ivory Coast, Oumar Farouk Comara (25).

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, makubaliano binafsi kati ya mchezaji huyo na Yanga tayari yamefikiwa. Kinachosalia kwa sasa ni klabu hiyo ya Jangwani kukamilisha mazungumzo na Golden Arrows kuhusu ada ya uhamisho ili dili hilo lifungwe rasmi.

Iwapo usajili huo utakamilika, Comara atakuwa nyongeza muhimu katika safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya Fred Ngoma, sasa macho na masikio ya mashabiki wa Yanga yanaelekezwa kwa Oumar Farouk Comara, ambaye anatajwa kuwa usajili unaofuata kutangazwa rasmi.