Home International BRIGHTON WAPINDUA MEZA, WATEMBEZA 5G

BRIGHTON WAPINDUA MEZA, WATEMBEZA 5G

LICHA ya Leicester City kuanza kupata bao la mapema kuongoza dakika ya kwanza halikuwapa nguvu ya kukusanya pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brigton.

Ni Kelechi Iheanacho alianza kupachika bao lakuongoza mapema kabisa kipindi cha kwanza dakika ya kwanza na bao la pili kwa timu hiyo lilifungwa na Patson Daka yeye alipachika bao la pili dakika ya 33 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Falmer.

Ni mabao ya Luke Thomas alijifunga dakika ya 10, Moises Caicedo alipachika bao dakika ya 15, Leandro  Trossard dakika ya 64 na Alexis Mac Allister alitupia mabao mawili dakika ya 71 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 90+7.

Ushindi huo wa mabao 5-2 waliopata Brighton unawafanya wakusanye jumla ya pointi 13 wakiwa nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 6 huku Leicester City wakiburuza mkiwa na pointi moja kibindoni.

Previous articleARSENAL WACHANA MKEKA
Next articleVIDEO:RAIS WA YANGA AWATAJA MABINGWA NDONDO CUP