Home International ARSENAL WACHANA MKEKA

ARSENAL WACHANA MKEKA

ARSENAL inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta imepoteza kwa mara ya kwanza msimu wa 2022/23 kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

Kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi kubwa watupiaji ni Antony dakika ya 35, Marcus Rashford huyu alitupia mawili dakika ya 66 na 75 kwa upande wa United.

Arsenal wao waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo bao la kufutia machozi lilifungwa na Bukayo Saka dakika ya 60.

Licha ya kichapo hicho Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sita huku Man United ikiwa nafasi ya tano na pointi 12.

Previous articleMABOSI SIMBA WACHARUKA,YANGA WAFUNGUKA USAJILI KISINDA
Next articleBRIGHTON WAPINDUA MEZA, WATEMBEZA 5G