Home Sports MZUNGU WA SIMBA USAJILI WAKE WAWAPA JEURI YA KUTWAA MATAJI

MZUNGU WA SIMBA USAJILI WAKE WAWAPA JEURI YA KUTWAA MATAJI

BAADA ya uongozi wa Simba kukamilisha usajili wa straika Mserbia, Dejan Georgijevic, mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Rage, amefunguka kuwa, msimu huu wanakwenda kurudisha mataji yote waliyopoteza msimu uliopita.

Simba imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ushambuliaji ambapo msimu huu wamekamilisha usajili wa viungo washambuliaji Nelson Okwa, Moses Phiri, Augustine Okrah na straika Dejan Georgijevic.

 Rage amebainisha kwamba: “Msimu uliopita haukuwa bora upande wetu, hii ilitokana na aina ya usajili ambao tulifanya, wachezaji wengi walishindwa kutupa kile ambacho tulitarajia huku wengine wakiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Msimu huu viongozi wetu wamejua wapi tuliteleza na aina ya usajili uliofanywa ni wazi tunakwenda kuwa tishio.

“Wachezaji waliosajiliwa msimu huu wote ni wazuri na nina uhakika tunakwenda kurudisha makombe yetu yote ambayo watani zetu Yanga wameyatwaa msimu uliopita, wachezaji wanapaswa kutambua kuwa wana deni kubwa kwa mashabiki, hivyo wanatakiwa kupambana katika mechi zote watakazocheza iwe nyumbani au kimataifa.”

Usajili wa Mserbia huyo unatajwa kuwa ni pendekezo la kocha Zoran Maki ambaye amemshusha mwamba huyo kama mbadala wa Chris Mugalu aliyesitishiwa mkataba wake kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri ukichangiwa na majeraha ya mara kwa mara.

Previous articleREAL MADRID WATWAA UEFA SUPER CUP
Next articleMASTAA HAWA YANGA NI DABI YAO YA KWANZA