Home International REAL MADRID WATWAA UEFA SUPER CUP

REAL MADRID WATWAA UEFA SUPER CUP

REAL Madrid wamebeba taji la UEFA Super Cup kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya EIntracht Frankfurt katika mchezo wa fainali uliokuwa na ushindani mkubwa.

 Ni mabao ya David Alaba dk 37 na Karim Benzema dk ya 65 yaliweza kuipa taji timu hiyo katika fainali iliyochezwa Uwanja wa Helnsiki usiku wa kuamkia Agosti 11.

Licha ya ushindi huo rekodi zinaonyeshwa kamba Real Madrid waliweza kutawala mchezo kwa asilimia kubwa ambapo waliweza kupiga jumla ya mashuti 13 kuelekea lango la wapinzani wao.

Katika mashuti hayo ni 7 yaliweza kulenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti 6 kuelekea katika lango la wapinzani na ni mashuti 3 yaliweza kulenga lango.

Pia umiliki wa mpira kwa Madrid ilikuwa ni asilimia 58 na wapinzani wao ilikuwa ni asilimia 42.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI
Next articleMZUNGU WA SIMBA USAJILI WAKE WAWAPA JEURI YA KUTWAA MATAJI