Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Aprili 19, 2026.
Tayari kikosi cha Simba SC kimewasili Dar kikitokea Arusha ambapo huko kimetoka kuvuna pointi 3 mbele ya Fountain Gate kwa ushindi wa magoli 3-0.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC amesema wanatambua mchezo ujao utakuwa mgumu wapo tayari kupambana kupata pointi tatu muhimu.
Namungo FC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 22 baada ya mechi 18 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili baada ya mechi 18 ikiwa na pointi 39.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku kwa wababe hawa kuwa katika msako wa pointi tatu muhimu.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.