Home Uncategorized BOCCO WA SIMBA AFUNGA BAADA YA SIKU 294

BOCCO WA SIMBA AFUNGA BAADA YA SIKU 294

MSHAMBULIAJI bora wa msimu wa 2020/21,John Bocco amefunga bao la kwanza kwenye ligi baada ya kuyeyusha jumla ya siku 294 bila kufunga.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho kwa Bocco kufunga ilikuwa Julai 18,2021 alipofunga bao lake la 16 mbele ya Namungo FC Uwanja wa Mkapa na kuibuka kuwa mfungaji bora.

Msimu wa 2021/22 ilikuwa ngumu kwake kuweza kucheka na nyavu baada ya kucheza mechi 16 na kutumia dk 639 bila kufunga.

Alifunga kwenye mchezo wake dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ni mchezo wa 17 kwake kucheza na alitumia dk 23 jumla katumia dk 662 uwanjani msimu huu kwenye ligi.

Pia beki Henock Inonga naye alifunga bao la kwanza ndani ya Simba ikiwa ni mchezo wake wa 16 kwa kuwa alicheza mechi 15 na kuyeyusha dk 1,235 bila kufunga.

@Dizo_Click.

Previous articleWACHEZAJI MUHIMU KULINDANA LALA SALAMA HII
Next articleYANGA:BADO TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO