Home Sports YANGA:BADO TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO

YANGA:BADO TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo za ligi.

Manara amesema kuwa kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zilizopita haina maana kwamba hawatakuwa imara

Yanga ni vinara wa ligi wanawania kutwaa Kombe la Ligi la 28 kwa kuwa wanayo 27 mpaka muda huu.

Jana walilazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Prisons kwa kugawana pointi mojamoja baada ya dakika 90.

“Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu nina amini kwamba Yanga itafanya vizuri kwa kufanyia kazi makosa ambayo yametokea na benchi la ufundi linajua ambapo wamekosea na watafanyia kazi hayo,”.

Previous articleBOCCO WA SIMBA AFUNGA BAADA YA SIKU 294
Next articleSPORTPESA YAKABIDHI MILIONI 50