Home Sports SPORTPESA YAKABIDHI MILIONI 50

SPORTPESA YAKABIDHI MILIONI 50

HATIMAYE Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, amemkabidhi Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, hundi ya Shilingi milioni 50 kama bonansi baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Ofisi za SportPesa Tanzania, zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam, mapema leo, ambapo Tarimba amewashukuru Simba kwa kuifikisha SportPesa katika hatua hiyo ya mashindano, huku akiwaomba kufanya hivyo tena msimu ujao ili waweze kuendeleza ile hali ya kuitangaza kimataifa zaidi.

“Napenda kuwapongeza viongozi na wachezaji wote wa Simba, kwa kuyafikia mafanikio na hatua ambayo mmepiga,kwani mmewapa heshima kubwa mashabiki wote wa Simba na SportPesa kwa ujumla wake, maana mmetuheshimisha kwa ukubwa jinsi mlivyoweza kutufikisha kimataifa na hatua nzuri kama hiyo.

“Niseme tu kuwa hii ni hatua nzuri na niaamini kwenye mashindano yajayo mtashiriki kwa kujipanga zaidi ili kufikia hatua kubwa zaidi ya hapa ili kutimiza lengo lenu kama timu,” amesema Tarimba.

Kwa upande wa Barbara yeye amesema kuwa: Nichukue hatua hii kuipongeza SportPesa kwa kutimiza kila makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wetu na zaidi nipongeze hili kwa kuendelea kutoa bonansi kubwa kama hii ya leo ya shilingi Milioni 50.

“Natambua kuwa SportPesa imekuwa ikitoa bonansi kila tunapofanikiwa kufanya jambo kubwa kwenye michuano mbalimbali, hivyo tunaamini SportPesa wamekuwa ni chachu kubwa kwetu katika kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kutoa bonasi tena kwa wakati bila kuchelewa,” amesema Barbara.

Previous articleYANGA:BADO TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO
Next articlePABLO:TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR