WACHEZAJI MUHIMU KULINDANA LALA SALAMA HII

    LALA salama huwa inakuwa na mambo mengi hasa kwa wachezaji kupambana kuweza kufikia malengo yao ambayo walikuwa wamejiwekea tangu mwanzo wa msimu.

    Hapa unaona wazi kwamba sio kwenye Ligi Kuu Bara pekee bali hata kwenye Ligi ya Wanawake na Championship huku mambo yanazidi kuwa ni moto.

    Hata kwenye Ligi ya Soka la Ufukweni pia mambo yanazidi kuwa na ushindani mkubwa tofauti na msimu uliopita.

    Hii ina maana kwamba kila kitu kipo tofauti kuanzia kwenye maandalizi pamoja na utendaji kazi kwa wachezaji pamoja na wachezaji wenyewe ambao wanatimiza majukumu yao.

    Kumekuwa na mwendo wa kusuasua kwa timu ndani ya uwanja kwa wakati huu huku nyingine zikipata matokeo hilo lipo wazi hivyo kwa zile ambazo bado hazina matokeo mazuri ni muhimu kujipanga upya.

    Muda wa lala salama ni muda wa kukamilisha hesabu kwa kuwa ukiachwa kidogo kurudi tena kwenye mwendo unaweza ukajikuta umeshaachwa na wale ambao wamekutangulia,

    Ambacho kinatakiwa ni kufanyia kazi makosa ambayo yamepita kwa mzunguko wa kwanza ili wakati huu wa mzunguko wa pili kuwa imara kwa kupata matokeo.

    Matokeo yanatafutwa na kinacholeta matokeo ni maandalizi mazuri kwenye kila mchezo hilo ni jambo la msingi na muhimu kuzingatia.

    Kwenye wachezaji ninapenda kutoa rai kwamba wakati wa kutimiza majukumu yenu tendeni haki kwa kufuata sheria zote 17 huku kila mmoja akiwa mlinzi wa mwenzake.

    Ile kasumba ya kutumia nguvu nyingi kwa wakati huu muda wake umekwisha na nina amini kwamba wakati huu ni muda wa kutumia zaidi akili kuliko nguvu.

    Kuharibiana kwa wachezaji kwa muda huu ni jamo baya na siku zote mchezo wa mpira si vita bali ni hesabu kali ambazo zinapangwa na kila timu ambayo inaingia uwanjani.

    Ipo wazi kwamba hakuna timu ambayo inaingia uwanjani ikiwa na hesabu za kupoteza mchezo kikubwa ambacho wanahitaji ni ushindi.

    Hivyo basi kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi ni muhimu kwa wachezaji kuamini kwamba ushindi unapatikana hata bila kuumizana.

    Jambo la msingi ni kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa ukamilifu akiamini kwamba mchezaji anapaswa kulindwa na sio kuumizwa ndani ya uwanja kisa msako wa ushindi.

    Kwa Championship pamoja na Ligi ya Wanawake pia bila kusahau Ligi ya Soka la Ufukweni muhimu kila mchezaji kuwa mlinzi kwa mchezaji mwenzake.

    @dizo_click.

    Previous articleHITIMANA:MBINU ZETU ZILIFELI KWA AZAM FC
    Next articleBOCCO WA SIMBA AFUNGA BAADA YA SIKU 294