Home Sports HITIMANA:MBINU ZETU ZILIFELI KWA AZAM FC

HITIMANA:MBINU ZETU ZILIFELI KWA AZAM FC

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa mbinu zao zilefeli kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC ubao uliposoma Azam FC 2-1 KMC.

Ni mabao ya Rodgers Kola ambaye alitupia mawili kwa Azam FC dk ya 1 na 36 na kufikisha mabao 7 kwenye ligi huku kwa KMC bao likifungwa na Miraj Athuman dk ya 48 likiwa ni bao lake la kwanza msimu huu.

Hitimana amesema kuwa walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kupata pointi tatu kwenye mchezo huo lakini walishindwa kutokana na nafasi ambazo walitengeneza kukosa.

“Ninaweza kusema kwamba mbinu zetu zilefeli mbele ya Azam FC hasa ile kushindwa kuzuia kufungwa ndani ya dakika 15 ikawa bahati mbaya tukafungwa bao dakika ya kwanza hii ilikuwa mbaya kwetu na tuliporudi kipindi cha pili tulikuwa imara.

Walipoona tunacheza kwa kasi hasa kipindi cha pili waliamua kuongeza beki mwingine ili aweze kusaidiana na Bruce Kangwa hilo likatufanya tushindwe kupata matokeo,hivyo tuna kazi ya kujipanga kwa mechi zijazo.

“Kwa hali ambayo wanayo Azam kwa sasa ni lazima ukipata nafasi uzitumiea na wao wakipata nafasi wanatumia lakini wametufunga mabao mepesi kweli,” amesema Hitimana.

KMC inabaki na pointi zake 24 baada ya kucheza mechi 22 huku Azam FC ikifikisha pointi 32 na imecheza mechi 22.

Previous articleMERIDIANBET YATOA MKONO WA PONGEZI KWA KINA MAMA WATAFUTAJI
Next articleWACHEZAJI MUHIMU KULINDANA LALA SALAMA HII