UONGOZI wa Yanga SC umebainisha kuwa wachezaji walijituma katika kusaka matokeo kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali licha yakupoteza dhidi ya Azam FC.
Juni 21, 2026 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Azam FC 3-2 Yanga SC kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup.
Matokeo hayo yanaipa tiketi Azam FC kutinga fainali huku Yanga SC ikipoteza taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kulitetea kwa muda wa miaka mitano mfululizo.
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema walikuwa wanahitaji kutwaa taji hilo lakini matokeo hayajawa upande wao.
“Kwa kilichotokea ni matokeo ya mpira, haikuwa bahati yetu hivyo tunakubali. Wachezaji wameonyesha jitihada kubwa na wamepambana kuhakikisha kwamba tunapata matokeo lakini haijafanikiwa.
“Tumetwaa taji hili kwa muda wa miaka mitano na tumepata ushindi kwenye mechi zetu ambazo zimepita, hivyo ilikuwa bahati ya Azam FC, tuna mechi nyingine na mashindano mengine tunajipanga kuwa imara zaidi,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.