RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa walikuwa bora kipindi cha kwanza lakini wakashindwa kuzitumia nafasi ambazo walizipata.
Usiku wa kuamkia leo ubao wa Uwanja wa Etihad ulisoma Manchester City 4-1 Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Ni mabao ya Kevin De Bruyne alitupia mawili dk 5 na 28 na Riyad Mahrez alitupia mawili dk 68 na 90+1 huku lile la United likijazwa kimiani na Jadon Sancho dk 22.
Rangnick amesema:”Nadhani tulikuwa bora kipindi cha kwanza lakini tumepoteza mchezo ni wajibu wetu kuweza kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.
Manchester United ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 47 huku City ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 69 kibindoni.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)