ABOUBAKAR AINGIA LEVO ZA ETO’O

NYOTA wa timu ya taifa ya Cameroon,Vincent Aboubakar kwenye mashindano ya Afcon 2021 nchini Cameroon yeye anakiwasha tu kwa kucheka na nyavu.

Mpaka sasa yeye ni namba moja kwa utupiaji ambapo amefunga jumla ya mabao matano kibindoni.

Timu ya Cameroon ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wamekuwa kwenye mwendo mzuri ambapo tayari wametinga hatua ya 16 bora.

Kwa mwendo ambao anakwenda nao anaingia anga za mshambuliaji mahiri wa zamani wa timu hiyo Samuel Eto’o ambaye aliwahi kufanya maajabu kwenye fainali za Afcon.

Nyota huyo wa Cameroon, amwfunga mabao matano katika mechi tatu za makundi kwenye Afcon 2021 na hakuna mchezaji mwingine wa Cameroon amefunga mara nyingi zaidi katika msimu mmoja wa fainali za Afcon sawa na Samuel Eto’o ambaye naye alifunga mabao matano kwenye mechi tatu.

Eto’o alifanya hivyo mwaka 2006 kwenye mechi tatu na akarudia tena mabao matano 2008.