IWAFIKIE mashabiki wa Simba kwamba tatizo la nahodha wa Simba kuwa kwenye kipindi kigumu cha kushindwa kufunga wala kutoa pasi ya bao kwenye ligi kwa msimu wa 2021/22 limepata dawa baada ya mshikaji wake Clatous Chama kurejea.
Chama alikuwa na maelewano mazuri na Bocco kabla ya kusepa msimu wa 2021/22 ambapo kwenye pasi mbili ambazo alitengeneza Bocco kwenye ligi mtu wa kwanza kuitumia na kujaza mpira kimiani alikuwa ni Chama.
Bocco alifanya hivyo msimu wa 2021/22 wakati Simba iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania na washkaji wote wawili walitokea benchi na kuweza kuipa pointi tatu timu ya Simba zama za Sven Vandenbroeck.
Kwa sasa Bocco ambaye anapambania tuzo yake ya ufungaji bora ambapo alifunga mabao 16 msimu uliopita bado hajafunga bao wala kutoa pasi na kinara wa kucheka na nyavu ni Fiston Mayele mwenye mabao sita na pasi moja ya bao.
Leo Bocco anatimiza siku ya 187 bila kufunga bao kwenye mechi za ligi na mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni Julai 18,2021 alipofunga mbele ya Namuno FC.