Home Sports BEKI KISIKI AONGEZA MKATABA YANGA

BEKI KISIKI AONGEZA MKATABA YANGA

YANGA wamemuongezea dili la mwaka mmoja kiraka wake Mkongomani, Yannick Bangala na kufikisha miaka miwili ya kuendelea kukipiga hapo.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zienee za kiungo mkabaji wa timu hiyo, Mkongomani Mukoko Tonombe kugomea kuuzwa TP Mazembe ya nchini DR Congo.

Bangala alijiunga na Yanga katika msimu huu akitokea FAR Rabat ya nchini Morocco baada ya kuvunja mkataba wa kuendelea kukipiga huko kabla ya kutua Jangwani.


Mmoja wa mabosi wa timu 
hiyo amesema kuwa, kiungo huyo wiki mbili zilizopita mabosi wa timu hiyo walimuongezea mkataba wa mwaka mmoja na kufikisha miwili baada ya ule wa awali kubakisha miezi sita.


Bosi huyo alisema kuwa 
viongozi wa timu hiyo walishtukia kiraka huyo kuwepo katika mazungumzo na klabu yake ya zamani ya FAR Rabat aliyokuwa anaichezea.

Aliongeza kuwa pia uongozi wa timu hiyo ulishtukia kuzidiwa ujanja na watani wao Simba na haraka kumuongezea mkataba wa kuendelea kubakia kukipiga hapo kwa misimu miwili.

“Yanga ipo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao imebakisha miezi sita na kati ya hao yupo Bangala ambaye tayari wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja.

“Bangala alisaini mkataba wa mwaka mmoja baada ya viongozi kuhofia kiwango chake, lakini baada ya kujiridhisha haraka wakamuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja na kufikisha miwili.

“Kikubwa viongozi walihofia kutokea kile kilichotokea kama cha Morrison (Bernard) ambaye walimpa mkataba wa miezi sita wakati inaelekea kumalizika haraka Simba wakamuwahi na kumsajili,” alisema bosi huyo.


Alipotafutwa Ofisa Habari 
wa timu hiyo, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa.

Chanzo:Championi

Previous articleMTIBWA YAWAITA SIMBA MANUNGU
Next articleABOUBAKAR AINGIA LEVO ZA ETO’O