MTIBWA YAWAITA SIMBA MANUNGU

THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa Simba wasiwe na mashaka kwa kuwa wanachokitaka wao ni mchezo huo uchezwe Uwanja wa Manungu.

Kesho,Januari 22 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar v Simba katika Uwanja wa Manungu.

Habari zinaeleza kuwa Simba wamewaeleza bodi kuwa wao wana mashabiki wengi jambo litakalokuwa tofauti kwao kutokana na uwanja huo kuwa na uwezo wa kubeba mashabi wachache.

Uwezo wa Uwanja wa Manungu ni kuingiza mashabiki 2,500 jambo ambalo limekuwa likileta mvutano kwa upande wa Simba.

Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco kimewasili Morogoro kwa maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kifaru amesema:”Tunataka kuona mchezo unachezwa kwenye uwanja wetu wa Manungu hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka tupo tayari na uwanja wetu ni mzuri, Simba wasiwe na wasiwasi,”.