Home International LEWANDOWSKI,RONALDO WASEPA NA TUZO

LEWANDOWSKI,RONALDO WASEPA NA TUZO

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Poland ambaye anakipiga Bayern Munich, Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa mwaka 2021.

Lewandowski, 33, ametwaa tuzo hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo ambapo katika kipindi hicho ametupia bao 69 akimshinda Lionel Messi na Mohamed Salah wa Liverpool.

Pia mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo yeye ametwaa tuzo maalumu.

Ronaldo ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa muda wote kimataifa. Lewandowski ni moja ya washambuliaji wenye ushkaji na nyavu alivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya miaka 49, ambapo alifunga goli 43 katika mechi 34 za Ligi kwenye kipindi kimoja cha msimu.

Kwa upande wa mchezaji bora upande wa Wanawake ni Alexia Puttellas ametajwa kuwa mchezaji bora wa FIFA.

Previous articleSIMBA YATAJA TIMU ITAKAYOTWAA UBINGWA
Next articleMORRISON AFUGUKIA ISHU YA KUSUGUA BENCHI