Home Sports MORRISON AFUGUKIA ISHU YA KUSUGUA BENCHI

MORRISON AFUGUKIA ISHU YA KUSUGUA BENCHI

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa, hana shida na kuanzia benchi ndani ya kikosi hicho, kwani ni jambo la kawaida kwenye timu yoyote kubwa na wajibu wake kama mchezaji ni kuhakikisha anaongeza jitihada kumshawishi kocha kumpa nafasi.

Tangu kiungo raia wa Senegal, Pape Sakho aanze kuuwasha moto ndani ya Simba, Morrison ameonekana kupata wakati mgumu kuanza kwenye kikosi cha timu hiyo.

Morrison aliuanza msimu huu akiwa kwenye fomu kubwa, huku akiisaidia Simba kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison alisema: “Kwenye timu yoyote kubwa lazima kuwe na changamoto ya ushindani wa namba hali ambayo inakuwa na faida kwa timu na kuongeza ubora kwa kuwa kila mchezaji habweteki bali lazima apambane kupata nafasi.

“Hivyo jambo kubwa ni kwamba ninafurahia kasi ambayo kama kikosi tumekuwa nayo na mafanikio ya kushinda Kombe la Mapinduzi. “Nipo tayari kupambana kuonesha uwezo wangu ili nipate nafasi ya kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza,”.

Jana Januari 17 wakati Simba ikifungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kiungo huyo alikuwa ndani ya uwanja na aliyeyusha dakika zote 90 huku Sakho akianzia benchi.

Previous articleLEWANDOWSKI,RONALDO WASEPA NA TUZO
Next articleAZAM WASEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA KWANZA