Home Sports AZAM WASEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA KWANZA

AZAM WASEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA KWANZA

Rodgers Kola amepachika bao mbele ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Bao hilo la ushindi amelipachika kimiani dakika ya 44 katika kipindi cha kwanza.

Jitihada za Mbeya Kwanza kuweza kuweka mzani sawa ziligonga mwamba katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Hata kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa Mbeya Kwanza kuweza kupata bao na kushuhudia dakika 90 wakipoteza pointi tatu mazima.

Inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 12.

Previous articleMORRISON AFUGUKIA ISHU YA KUSUGUA BENCHI
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO