Home Sports SIMBA YATAJA TIMU ITAKAYOTWAA UBINGWA

SIMBA YATAJA TIMU ITAKAYOTWAA UBINGWA

KOCHA wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa kwa upande wako anaona Azam FC wanayo nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa siku za mbeleni kutokana na kikosi chao kuimarika kila siku.


Pablo amesema amekutana na Azam 
FC kwenye mechi mbili kwa siku za hivi karibuni na ameona kuna utofauti mkubwa kwenye mechi ya kwanza na ya pili ambayo wamecheza na anaona kabisa timu ina ari ya kuwa bingwa.

“Wana vijana wengi wenye vipaji na baada ya muda mfupi kila kitu kitakwenda sawa. Timu yao nzuri sana pengine kuliko watu wanavyofikiria,” alisema.


Simba walikutana na Azam FC, 
kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Kabla ya hapo walikutana kwenye ligi kuu na kuvuna ushindi wa 2-1

Simba jana ilionja joto ya jiwe kwa kupoteza mchezo wa kwanza ndani ya ligi baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City Mtupiaji wa bao la ushindi alikuwa ni Paul Nonga aliyejaza kimiani bao hilo dakika ya 19.

Previous articleLIGI KUU BARA KUENDELEA MBEYA,PALEPALE SOKOINE
Next articleLEWANDOWSKI,RONALDO WASEPA NA TUZO