Home International ARTETA AKASIRISHWA KUTOLEWA KOMBE LA FA

ARTETA AKASIRISHWA KUTOLEWA KOMBE LA FA

MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa ni maumivu makubwa wameyapata baada ya kupoteza mbele ya Nottm Forest na kutolewa kwenye Kombe la FA.

Katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la FA ubao wa Uwanja wa City Ground ulisoma Nottm Forest 1-0 Arsenal.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Lewis Grabban dakika ya 83 na kuwafanya waweze kusonga mbele huku Arsenal ikifungashiwa virago.

Kocha huyo amesema:”Ni maumivu makubwa ambayo tumeyapata baada ya kupoteza mchezo wetu na kuondolewa kwenye Kombe la FA,” .

Kwenye mchezo huo Arsenal iliweza kupiga jumla ya mashuti 10 huku katika hayo hakuna hata moja ambalo lililenga lango na wapinzani wao walipiga mashuti 7 na ni matatu ambayo yalilenga lango.

Previous articleMOTO WA KIBU DENNIS HAUPOI
Next articleMTAMBO WA MABAO YANGA WAANZA KAZI