Home Sports AJIBU KUIKOSA SIMBA LEO KWA MKAPA

AJIBU KUIKOSA SIMBA LEO KWA MKAPA

KIUNGO Ibrahim Ajibu ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC kuna uwezekano asianze kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba ambao ni wa Ligi Kuu Bara.

Timu zote mbili zimeweka wazi kwamba zinahitaji pointi tatu muhimu ambapo kwa upande wa Azam FC, Idd Aboubakhari, Kocha wa Makipa wa Azam FC amesema kuwa wanatambua Simba
ni timu kubwa na wanawaheshimu ila watapambana kupata ushindi.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri, tumetazama mechi zao na ninatambua kwamba wao watakuwa
wametufuatilia, dakika 15 za mchezo zile za mwanzo itakuwa ni kwa ajili ya kusoma mbinu za wapinzani wetu kisha
tutajua nini tutafanya.

“Ujio wa Ajibu ni mipango ya benchi lakini kusema kwamba anaweza kuanza itakuwa ngumu kwani mipango ya timu huanza muda mrefu ikiwa tutamchezesha labda inaweza kuwa sapraizi.

“Kuhusu kutokuwepo kwa Never Tigere, Prince Dube ambao wapo kwenye timu ya taifa sio tatizo kwani tuna wachezaji 30 na hao waliopo kwenye majukumu mengine kwenye timu zao za taifa tunawaombea kheri,” amesema.

Previous articleSIMBA SC V AZAM FC MWENDO WA HESHIMA, AJIBU OUT
Next articleADHABU ZATOLEWA NA BODI YA LIGI