ABOUTWALIB Mshery ingizo jipya ndani ya Yanga linatarajiwa kuweza kuanza kazi leo Desemba 31 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.
Mshery amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake pale Morogoro kwa ajili ya kuweza kupata changamoto mpya.
Baada ya usajili wake kukamilika alianza mazoezi na wachezaji wenzake ambao walimkaribisha kwa kuimba na kucheza kisha ikwa ni mwendo wa mazoezi.
Kutokana na kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kusepa kuelekea kwenye timu ya taifa ya Mali kwa ajili ya maandalizi ya Afcon Mshery huenda akaanza kwenye mchezo wa leo.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi aliweka wazi kwamba anatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa lakini wao wanahitaji pointi tatu.
Kipa mwingine ambaye amebaki ndani ya Yanga ni Eric Johola ambaye huyu ni chaguo namba mbili.