>

AUBA MAJANGA,AVULIWA UNAHODHA

KLABU YA Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imemvua unahodha Pierre-Emerick Aubameyang na hatacheza kwenye mechi ya ligi dhidi ya West Ham kesho Jumatano usiku.

Raia huyo wa Gabon kwake inakuwa ni majanga kuvuliwa kitambaa hicho pamoja na mwendo wake kuwa wa kusuasua kwa msimu wa 2021/22.

“Kufuatia ukiukaji wake wa nidhamu wiki iliyopita, Pierre-Emerick Aubameyang hatakuwa tena nahodha wa klabu yetu, na hatazingatiwa kwenye uchaguzi wa kikosi kitakacho cheza mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham United.

“Tunatarajia wachezaji wetu wote, haswa nahodha wetu, kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na viwango ambavyo sote tumeweka na kukubaliana. Tunaangazia kikamilifu mechi ya kesho,” ilieleza taarifa hiyo.