VIZINGITI VYA MABAO SIMBA V YANGA

    KUMEPOA mtaani kama hakuna kilichotokea vile baada ya dakika 90, Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-0 Yanga na kufanya asiwepo mbabe.

    Hapa tunakuletea vizingiti vilivyosababisha mambo kuwa hivyo namna hii:-

    Manula

    Aliokoa hatari dk ya tano shuti la Jesus Moloko pia aliweza kuwa kizingiti kwa Moloko dk ya 49, dk ya 58 aliokoa hatari ya Ntibanzokiza, dk 87 alikuwa kizingiti kwa Yanick Bangala

    Inonga

    Dk 3 aliokoa hatari ya Fiston Mayele aliyekuwa anakwenda kwenye lango

    Bernard Morrison

    Dakika ya 7 alipiga shuti lililokwenda nje ya lango akiwa nje kidogo ya 18 kwa pasi ya Meddie Kagere pia dk ya 19 alipiga shuti akiwa nje ya 18 ambalo lilikwenda nje ya lango

    Mkude

    Jonas Mkude dk ya 22 alimpoka mpira Feisal Salum aliyekuwa kwenye mmiliki wa mpira, dk 54 aliokoa kona ya Ntibanzokiza ndani ya 18, dk ya 70 alikuwa kizingiti kwa Fei na aliweza kuonyeshwa kadi ya njano

    Kanoute

    Sadio Kanoute alikoka mpira wa Said Ntibanzokiza dk 22 kwa kichwa na uliokuwa unakwenda kwenye lango la Manula pia dk ya 87 alikuwa kizingiti kwa Ntibanzokiza aliyepiga pigo huru

    Onyango

    Joash Onyango dk 22 alilazimika kutumia mikono kumzuia Mayele aliyekuwa analisaka lango la Manula na kwa kitendo hicho alionyeshwa kadi ya njano.

    Dakika ya 42 Onyango aliweza kumdhibiti Mayele asimtungue Manula ambaye aliteleza katika harakati za kuokoa.Dakika ya 46 aliweka kizingiti kwa Ntibanzokiza aliyefanya jaribio ndani ya 18.

    Atajilaumu mwenyewe dk ya 85 ambapo alipiga shuti la hovyo lililokwenda nje ya 18 katika lango la Diarra

    Kapombe

    Shomari Kapombe alikuwa kizingiti kwa Ntibanzokiza dakika ya 33. Dakika ya 55 aliokoa pigo la Ntibanzokiza ndani ya 18 kwa kichwa na kuwa kizingiti kwa Yanga kupata bao.

    Kagere

    Meddie Kagere akiwa kwenye umiliki wa mpira dakika ya 39 ndani ya 18 alipiga shuti la hovyo ambalo lilikuwa kizingiti kwa timu yake kupata bao.

    Hassan Dilunga

    Kiungo huyu atajilaumu mwenyewe dk ya 90 kwa shuti lake ambalo lilikuwa kizingiti kwa Simba kupata bao kwa kuwa lilikwenda nje ya 18.

    Yanga

    Diarra

    Diarra Djigui kipa wa Yanga dk ya 45 aliweza kuokoa kichwa cha Meddie Kagere ndani ya 18 na kuwa kizingiti kwa Simba kufunga na dk 45 pia aliweza kuokoa shuti la Hassan Dilunga na dk ya 87 alikuwa kizingiti kwa Kanoute ambaye alifanya jaribio akiwa nje ya 18

    Dakika ya 57 alikuwa kizingiti kwa Morrison ambaye alipiga shuti lililolenga lango akiwa ndani ya 18

    Job

    Dickosn Job dk ya 12 alimzuia Morrison kuingia ndani ya 18 na kumchezea faulo ambayo haikuzaa matunda kwa Simba pia alimzuia Morrison dk 42 pia dk ya 59 alimpa tabu Morrison na alionyeshwa kadi ya njano.

    Dakika ya 46 aliokoa hatari ya Mohamed Hussein iliyokuwa inakwenda kwenye lango lao.

    Kibwana Shomari

    Morrison aliwekwa kwenye kizingiti chake dk ya 67 na 74

    Aucho

    Khalid Aucho kiungo msumbufu dk ya 23 alipiga kichwa kilichokwenda nje ya lango akiwa ndani ya 18 kwa faulo iliyopigwa na Said Ntibanzokiza.

    Mayele

    Dakika ya 27 akiwa ndani ya 18 alikosa utulivu kwa kushindwa kuitumia pasi Feitoto, dk 42 alikwama kumtungua Manula ambaye alitoka kwenye lango.

    Feisal

    Kiungo Feisal Salum dakika ya 56 alimzuia Sadio Kanoute kulifuata lango la Diarra na kwa kitendo hicho alionyeshwa kadi ya njano.

    Mwamnyeto

    Bakari Mwamnyeto dk ya 57 alimpunguzia kasi Morrison aliyekuwa akilifuata lango la Diarra pia dk ya 78 alikuwa kizingiti kwa Kagere

    Djuma

    Djuma Shaban beki wa Yanga dk ya 57 alikuwa kizingiti kwa Mohamed Hussein ambaye alikuwa anataka kupeleka salamu Yanga

    Previous articleSIMBA:HAPA KAZI TU
    Next articleAUBA MAJANGA,AVULIWA UNAHODHA