MSHAMBULIAJI wa zamani wa AS Vita na Orlando Pirates, Jean Marc Makusu Mundele, ameweka wazi kuvutiwa na timu za Simba na Yanga huku akiweka wazi yupo tayari kujiunga na mojawapo ya timu hizo.
Makusu kwa sasa anakipiga DC Motema Pembe ya DR Congo mara baada ya kuwa na maisha magumu ndani ya Orlando Pirates.
Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka nchini DR Congo, Makusu alisema licha ya kuwahi kuhitajika ndani ya klabu hizo na kushindwa kujiunga nazo, lakini anaamini kwa sasa ni wakati sahihi kwake kuzichezea.
“Simba na Yanga ni timu kubwa na nzuri, zote nazifahamu kwa kuwa Simba nimeshawahi kukutana nao wakati nikiwa AS Vita, Yanga naifahamu kwa kuwa kuna marafiki zangu pale kama Yanick Bangala na Djuma Shabani.
“Mara kwa mara nimekuwa nikisikia tetesi juu ya Simba na Yanga, hapo awali Simba iliwahi kuleta ofa na Yanga
pia, lakini ilishindikana, bado nafasi ipo na kama ikitokea watanihitaji naamini itakuwa sahihi kwangu kujiunga ndani ya timu hizo,” alisema Makusu.