NABI AKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI

IKIWA zimebaki sikutatu kabla dirisha dogo la usajili hapa nchini halijafunguliwa, uongozi wa Yanga umefunguka kuwa katika kuhakikisha wanafanikisha mpango wao wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, umejipanga kukiongezea nguvu kikosi hicho kwa kushusha majembe mapya, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi akiwa mwamuzi wa mwisho.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu na kudumu kwa takribani mwezi mmoja.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinus, alisema: “Baada ya
kukamilisha mchezo wetu dhidi ya Simba, shughuli kubwa ya kiutendaji tutakayokuwa nayo ni juu ya maboresho ya kikosi chetu kupitia dirisha dogo la usajili ambapo tayari tutakuwa tumepokea ripoti ya mwalimu.

“Katika kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kwa asilimia 100 usajili wa dirisha hili, kuendana na ripoti ya mwalimu kuna nyota ambao watatolewa kwa mkopo, lakini pia tutasajili mchezaji yeyote ambaye kocha atampendekeza,” .

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi nane.