ISHU YA UBINGWA MABOSI SIMBA WAKAA KIKAO NA PABLO

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ulikaa kikao na Kocha Mkuu, Pablo Franco kujadili malengo ya timu hiyo ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara

Kocha huyo jana Desemba 5 likiongoza kikosi hicho ugenini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows na aliweza kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi.

Baada ya dakika 90 Uwanja wa Heroes uliopo Zambia uliweza kusoma Red Arrows 2-1 Simba na mtupiaji alikuwa ni Hassan Dilunga, lakini Simba iliweza kutinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 4-2 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilishinda mabao 3-0.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa walikaa kikao na kocha huyo kumpa malengo ya timu na wanaimani kwamba kila kitu kitakamilika.

“Hatukufanya maamuzi ya ghafla lakini kikubwa ambacho tulikuwa tunahitaji ni kuona matokeo mazuri, tulifanya kikao na Pablo, (Franco) na kumwambia malengo yetu ya timu ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi.

“Ili kuweza kutwaa ubingwa ipo wazi kwamba kinachohitajika ni ushindi kwenye mechi ambazo tutacheza na ligi ni ngumu kwa kuwa yeye ni mwalimu na wachezaji wapo tayari basi tunaamini kwamba jukumu hilo litatimia.