DUH!KUMBE KUNA TIMU IMEFUNGWA NA YANGA MABAO 800

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao,(Simba) ni timu pekee ambayo imefungwa mabao mengi na Yanga jambo ambalo haliwapi presha kuelekea mchezo wao.

Desemba 11, Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Manara ameliambia Championi Jumatatu kuwa ukitafuta timu ambayo imefungwa mabao mengi na Yanga ni timu yao, (Simba) jambo ambalo linawapa nguvu kuelekea mchezo wao.

“Kwani hivi tunakutana nao lini yaani wale jamaa zetu? Maana ukiangalia kwa mujibu wa rekodi hakuna timu ambayo Yanga tumeifunga mabao mengi zaidi ya 800 timu ile, (Simba).

“Ukiangalia rekodi timu ambayo imefungwa kwenye mechi nyingi kila tunapokutana hakuna hakuna ni wao sasa unadhani katika mechi yetu tutakuwa tunaogopa? Hapana ninachowaambia mashabiki ni kwamba Yanga ina watu wa kazi na tunachohitaji ni ushindi,” .

Kwa sasa kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kikiwa kipo kambini Kigamboni na miogoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye maandalizi ni pamoja na Feisal Salm, Kibwana Shomari, Said Ntibanzokia na Zawad Mauya.