Home Sports MBEYA CITY YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0

MBEYA CITY YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0

MBEYA City leo imeichapa mabao 2-0 Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ni mabao ya Hussein Masalanga dakika ya 42 liliweza kuwafanya Dodoma Jiji kuduwaa kwa muda wakiwa hawajaweza kufunga bao la kuweka mzani sawa.

Dakika 45 za kipindi cha pili huko mambo yalizidi kuwa magumu kwa Dodoma Jiji ambao jitihada zao ziligonga mwamba katika kusaka bao.

Msumari wa mwisho kwa Mbeya City ulihitimishwa na nyota wao Paul Nonga ilikuwa dakika ya 88 na kufanya kazi ikamilike kwa Mbeya Citu kuweza kuituliza Dodoma Jiji inayonolewa na kocha Mbwana Makata.

Sasa Mbeya City inakuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14 huku Dodoma Jiji ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 12.

Previous articleDUH!KUMBE KUNA TIMU IMEFUNGWA NA YANGA MABAO 800
Next articleBREAKING:ORODHA YA WAAMUZI WA SIMBA V YANGA HII HAPA