KIKOSI cha Simba kwa sasa kipo nchini Zambia ambapo kimewasili jana Desemba 3 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Desemba 5 ambapo utakuwa ni wa marudio baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba kushinda mabao 3-0.
Kitu pekee ambacho kwa sasa Simba wanahitaji ni ushindi wa aina yoyote ile ama sare ili waweze kusonga mbele, ikiwa wataruhusu kufungwa mabao zaidi ya matatu safari yao itakuwa imegota hapo kimataifa.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wameweza kuchukua tahadhari zote kuhusu Corona.
“Timu ipo salama na kla mchezaji anamorali kubwa ya kuweza kufanya vizuri na kupata matokeo chanya, kwa kuwa ushindi ni jambo la muhimu.
“Kuhusu tahadhari ya Corona tumekuwa tukifanya hivyo tangu tukiwa Tanzania hivyo huku pia tunaendelea kuchukua tahadhari kwani ni lazima tufuate taratibu ambazo zimewekwa,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo na kikosi ni pamoja na Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu, Meddie Kagere,Jonas Mkude.